![]() |
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema watu 152 watafikishwa mahakamani
mkoani Njombe kutokana na kujiandikisha mara mbili katika Daftari la
Kudumu la Wapigakura kwa mfumo mpya wa ‘Biometric Voter Registration
Kit’ (BVR).
Aidha,
imeeleza kuwa kata 130 zimeongezeka kutokana na Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kufanya mabadiliko ya kiutawala katika
kata, vijiji,vitongoji na Mitaa hivyo kulazimu NEC kuhairisha kwa wiki
moja uandikishaji wa daftari uliokuwa ukianza jana kwa baadhi ya mikoa.
Kaimu
Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dk Sisti Cariah alisema hayo jana wakati
akielezea kuahirishwa kwa wiki moja uandikishaji hadi Juni 16 mwaka huu
kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Mara.
Akizungumzia
suala la watu kujiandikisha mara mbili, alisema katika mkoa wa Njombe
ambao Daftari hilo liko tayari na wiki ijayo litawekwa wazi kwa siku
tano na kisha kufanyiwa marekebisho kwa siku moja na wamebaini watu 152
waliojiandikisha mara mbili.
Alisema
watu hao wametenda kosa la jinai na watashtakiwa, huku akitoa onyo kwa
watu kuacha kufanya hivyo kwani mashine za BVR zinagundua
wanaojiandikisha zaidi ya mara moja.
Alisema wataweka wazi baadhi ya watu waliojiandikisha mara mbili kwenye mikoa yote, ambayo iko tayari.
Alisema
mpaka sasa tayari wamepokea madaftari yaliyokamilika ya uandikishaji
kwa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma huku uandikishaji huo ukiwa
umekamilika kwa asilimia 50 na wanatarajia kukamilisha uandikishaji
mwezi Julai.
|
June 12, 2015
150 KORTINI KWA KUJIANDIKISHA MARA MBILI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGAKURA KWA MFUMO MPYA BVR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment