![]() |
| Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe
(pichani) , amenusurika kifo baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kutoka
Iringa kwenda Zanzibar kutaka kugongana uso kwa uso na ndege nyingine
dakika moja kabla ya kutua.
Waziri Membe akiwa na ujumbe wake wa watu wanane, walikuwa
wakisafiria ndege ya kukodi kampuni ya 5H NEG Precition Aviation
ikirushwa na rubani Mathew Mhahiki, ambaye ameonyesha kushangazwa na
tukio hilo alilodai “ni kwa rehema za Mungu tumepona ajali hii.”
Akizungumza na gazeti hili, rubani Mhahiki alisema: “Lazima kuna
tatizo katika control center hata hivyo tayari nimeongea nao na
wameniomba samahani na kudai walipitiwa, maana kwa hali ilivyokuwa ni
kwamba tungegongana wakati wa kutua maana nimeshangaa tu kuona ndege hii
hapa ndiyo maana nikaamua kumkwepa mwenzangu nikapanda juu.”
Waziri Membe alisema: “Nina uzoefu mkubwa wa kusafiri na ndege
mahali pengi duniani, hali hii ilikuwa ni ajali na labda sasa tungekuwa
dead bodies, lakini ninajua Mungu yuko upande wetu katika safari hii ya
uhakika, lakini pia izingatiwe nimekuja kufanya kazi ya Mungu.”
“Katika safari hii tutashuhudia mambo mengi sana, lakini kwa kuwa
kila ninapotaka kuondoka nyumbani ama hotelini mara nyingi nimekuwa
nikimtanguliza Mungu maana bila Mungu hii ilikuwa ni mwisho wa maisha
yetu tuliokuwa kwenye ndege hii.”
Naye mwanasiasa anayenyemelea ubunge Jimbo la Rungwe Mashariki,
Richard Kasesela, aliyeongozana na Waziri Membe ameonyesha wasiwasi wa
hali hiyo kuwa inaweza kuwa ni hujuma dhidi ya Membe.
Waziri Membe alikuwa amealikwa mjini hapa na Umoja wa Akimama wa
Kikristu (Umaki) wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar waliokuwa
wakifanya mkutano wao mkuu unaofanyika kila baada ya miaka mitano
akitokea Iringa ambako alikwenda kutafuta udhamini wa chama ili
kumwezesha kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM.
Akiwa uwanjani hapo, Waziri Membe alikutana na Naibu Waziri wa
Fedha, Mwigulu Nchemba aliyekuja hapa Zanzibar kutafuta wadhamini ambapo
makada hao walipata nafasi ya kuzungumza.
Akiwa katika mkutano huo, Waziri Membe alisema: "Miongoni mwa mambo
yanayonikera ndani nafsi yangu ni kuona mwanamke bado anaachwa nyuma,
hili halipendezi, ni lazima tuhakikishe wanawake wanapata elimu ya
ufundi stadi maana mwanamke akiwezeshwa hasa katika eneo hili la elimu
wanaweza hata kushinda wanaume wengi.”
|
June 12, 2015
NDEGE YA MEMBE YANUSURIKA AJALI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment