![]() |
| Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba (pichani), Jumapili anatarajiwa kuchukua fomu ya kugombea urais.
Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo, alisema
jana kuwa mchakato wa kutangaza nia ya kugombea urais ulianza Mei 10
hadi Juni 10, mwaka huu na kuwa hadi kufikia jana ambayo ilikuwa siku ya
mwisho walikuwa wamepokea jina Lipumba pekee.
“Mchakato wa utangazaji nia ya kugombea ndani ya chama ulifunguliwa
Mei 10 na hadi kufikia jana, tumepokea jina la Prof. Lipumba tu katika
ngazi ya urais,” alisema.
Aidha, alisema walipanga wagombea waliotangaza nia ya kugombea
urais kuchukua fomu kuanzia Juni 11, mwaka huu, lakini kwa kuwa mgombea
mmoja ndiye amejitokeza wakapanga Juni 14, 2015 iwe siku ya mwisho
kuchukua fomu kwa ngazi hiyo.
Alisitiza kuwa wananchama na wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa
wingi kwenda kumsikiliza Prof. Lipumba ambaye ataeleza kwa nini
amechukua fomu kugombea urais.
Aliongeza kuwaBaraza la Kuu la Uongozi la chama hicho linatarajiwa
kukutana Julai 11 na 12, mwaka huu kwa ajili ya uteuzi wa mwisho wa
wagombea katika ngazi ya ubunge na urais na kuwa hadi Julai 20, mwaka
huu vyama vyote vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
vimekubaliana viwe vimemaliza kuteua wagombea ambao watapitishwa katika
vikao vya Ukawa.
Mketo alisema katika majimbo 189 ya Tanzania Bara, tayari
wameshapata wagombea waliotangaza nia ya kugombea kwenye majimbo 133
wakati 56 bado hayajatangaziwa nia.
|
June 12, 2015
PROF. LIPUMBA KUCHUKUA FOMU YA URAIS JUMAPILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment