KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 16, 2015

AHADI ZA RAIS KIKWETE ZAWATESA WABUNGE CCM.

Mbunge wa Magu, Dk. Festus Limbu.                                                 
Ahadi zilizotolea na Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 zinawatesa wabunge wengi wa CCM kutokana na baadhi kutokamilika.
 
Hali hiyo ilijitokeza jana bungeni katika kipindi cha maswali na majibu, wakati wabunge wengi walihoji ni lini ahadi hizo zitakamilika.
 
Akiuliza swali la nyongeza,  Mbunge wa Magu, Dk. Festus Limbu (CCM), alitaka kujua ni lini serikali itatekeleza ni mradi wa maji katika mji wa Magu.
 
Naye Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM), alitaka kujua ni lini serikali itatimiza ahadi mbalimbali za ukamilishaji wa miradi ya maji katika jimbo hilo.
 
“Kuna ahadi nyingi ambazo zilitolewa na Rais Jakaya Kikwete, lakini cha kushangaza miradi hiyo haijatekelezwa, sasa ni lini serikali itakamilisha ahadi hizo” aliuliza na kuongeza:
 
“Naitaka serikali itoe kauli ni lini itatekeleza ahadi hizo ili wananchi waondokane na adha ya maji ambayo inawafanya kushindwa kufanya shughuli nyingine za maendeleo.” 
 
Akijibu, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, alisema ahadi zote zilizotolewa na rais zitatekelezwa.
 
Hata hivyo, alisema tatizo kubwa ambalo linasababisha baadhi ya miradi kutokutekelezeka kwa wakati ni ufinyu wa bajeti.
 
Alisema serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inakamiliswa ukosefu wa fedha za kutosha imebaki kuwa changamoto kubwa.

No comments:

Post a Comment