![]() |
MSANII
aliyerejea na kutikisa na wimbo wa 'Mwana', Ali Kiba, amesema kung'ara
kwake katika Tuzo za Muziki wa Tanzania (KTMA) 2015 kumetokana na kazi
nzuri aliyoifanya na si mipango ya nyuma ya pazia kama inavyodaiwa.
Mkali
huyo wa muziki wa kizazi kipya alitwaa tuzo sita katika hafla ya KTMA
2015 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani Citry jijini Dar es Salaam
Jumamosi usiku akimbwaga mpinzani wake, Diamond Paltinumz aliyeambulia
tuzo tatu.
Baada ya
ushindi huo wa kishindo, kuliibuka maneno mengi mitaani kwamba ushindi
wa Ali Kiba dhidi ya Diamond ulitokana na kubebwa.
Hata
hivyo, akizungumza na waandishi wa habari mfupi baada ya kutua jijini
hapa leo alfajiri akitoka Marekani Ali Kiba amepuuza madai hayo na
kueleza kuwa kung'ara kwake kumetokana na kazi nzuri aliyoifanya kupitia
wimbo wake wa 'Mwana'.
"Nina
haki ya kutwaa tuzo nyingi hizo kutokana na kazi nzuri. Wimbo wangu
(Mwana) ulikuwa mzuri na kiwango kimeongezeka," amesema Ali Kiba.
Aidha, msanii huyo amesema video ya wimbo wake wa 'Cheketua' imekamilika na itatoka ndani ya wiki hii.
"Video ya
'Mwana' ilizungumzwa tofauti na kila aliyeiangalia. Mtayarishaji wa
'Cheketua' si ytule aliyetengeneza video ya 'Mwana'. Kikubwa mashabiki
wangu wategemea kitu kizuri," amesema zaidi Ali Kiba.(VICTOR)
|
June 19, 2015
ALI KIBA: NILISTAHILI TUZO SITA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment