Balozi,
Patrick Chokala akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais kupitia Chama Cha
Mapinduzi(CCM) leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar
es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mwandishi
wa Habari wa Rais wa awamu ya Pili, BaloziPatrick Chokala ametangaza
nia ya kugombea urais ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ili aweze
kupeperusha bendera hiyo katika uchaguzi mkuu ujao mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo
jijini Dar es Salaam, Balozi Chokala amesema umefika wakati wa kurejesha
haki kwa wananchi ili wawe na imani na uongozi na pia kuwa na ari ya
kuleta maendeleo.
Amesema
katika kutekeleza miradi inapaswa kutumia watalaam wa elimu ya jamii
kikamilifu kabla ya kutekeleza kama mradi wa gesi ambao ilileta vurugu
katika mikoa ya Kusini wakati serikali ilikuwa ina nafasi ya kuelewesha
wananchi.


No comments:
Post a Comment