
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), akiwasilisha kwa Rais wa Burundi, Mhe. Pierre Nkurunziza maamuzi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 31 Mei, 2015 Jijini Dar es Salaam. Mhe. Mwakyembe aliongoza ujumbe wa Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ziara ya kikazi nchini Burundi tarehe 15 Juni, 2015.

Rais Nkurunziza akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula walipowasili kwa ajili ya kuzungumza nae.



No comments:
Post a Comment