KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 27, 2015

AU YATAKA JASUSI WA RWANDA AACHIWE MARA MOJA

Umoja wa Afrika umetaka  kuachiwa huru mara moja kwa  Jasusi Jen karenzi Karake aliyekamatwa London Jumamosi iliyopita .

Katika mkutano wa dharura umoja wa Afrika  uliofanyika jumatano katika Makao Makuu ya Umoja huo yaliyopo mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa , ,umelaani kukamatwa kwake na kuitwa ni uvunjifu wa sheria.

Jana kwa kuonyesha mshikamano  Rwanda imeungwa mkono sana umoja Afrika,siku mbili baada ya kupokea ombi kutoka Rwanda baada ya Jen  Karake kukamatwa.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo, alisema kukamatwa  kwa Karake ni makosa kwa Rwanda na Afrika kwa ujumla

“Upuuzi wa jambo lenyewe ni kwamba waliohusika na mauaji ya kimbari  wameshitakiwa kwa mujibu wa sheria mbalimbali za kimataifa,  wengi wao hivi leo miaka 22 baadaye wanaishi huru na kuzunguka zunguka
miji mikuu ya Ulaya na wanaweza kuwarubuni majaji wa washitaki waliosimamisha mauaji ya kimbari,huu ni upuuzi kabisa ,” alisema Mushikiwabo
.
1435356291Loiuse-Mushikiwabo-(2)
Waziri Louise Mushikiwabo

Akielezea jinsi alivyo kamatwa Jen Karake Waziri  Mushikiwabo anasema kuwa inashangaza kwamba amekamatwa baada ya kusafiri kwenda Uingereza mara kadhaa , na kusisitiza kuwa hakuna uhusiano na mashtaka ya Uhispania

 “Swali ni kwamba ,kwa nini iwe sasa? kitu gani hasa kilichofanya mashitaka hayo yadumu kwa mda mrefu 

Akizugumza na waandishi wa habari  ,Waziri huyo alisema AU inapaswa  kufanya kila  unachoweza kummaliza uonevu huo  wa kisheria kujiingiza katika maajalidiano ya kisiasa ili kuakikisha haki inatendeka sawa

Akijibu maoni kwamba nchi za Ulaya zimetimiza haki yao kisheria, alisema haki ya miaka 22 ya mauaji ya Watutsi huo ni mfano mbaya.

“Kuna mifano mingi inayoonyesha mwingiliano  wa siasa na haki kama ni hivyo , kwanini sisi Rwanda  tunawaomba hao wanao fuata sheria na walioendelea kuwarudisha nyumbani waliohusika na mauaji ya kimbari ? kesi ya Jen. Karenzi hivi leo ni uvunjaji mkubwa wa haki.

Kamishna wa  AU amani na usalama Balozi. Smail Chergui, alieleza kwamba  kukamatwa kwa kiongozi huyo kunapaswa kuliamsha bara la Afrika kujihusisha na ukamatwaji huo
Katika kuonyesha mshikamano,nchi nyingine za Afrika Mashariki zilimsindikiza Waziri huyo wa Rwanda kwenye mkutano huo 

No comments:

Post a Comment