KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 29, 2015

EDWARD LOWASSA APATA WADHAMINI MKOA WA DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Ramadhan Madabida akizungumza jambo kumuhusu, Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (kulia), wakati alipofika kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam kusaini kitabu  wakati akiwa katika ziara yake ya kutafuta saini za WanaCCM wakumdhamini ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 212, 150 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi ya WanaCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakimshangia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Ramadhan Madabida (hayupo pichani) .             
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, Mkewe Mama Regina Lowassa pamoja na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu wakiwa sambamba na wanaCCM wengine wakati wakiwasili kwenye Ofisi za CCM Tawi la Ilala Kota, Mchikichini jijini Dar , Juni 27, 2015.                           
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Ernest Chale akikabidhi fomu za Wadhamini kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa Juni 27, 2015. Jumla ya WanaCCM 44,299 wa Wilaya ya Ilala Wamemdhamini Mh. Lowassa ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.    

No comments:

Post a Comment