![]() |
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimesema kimesikitishwa sana na kitendo cha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama cha Wananchi (CUF) kususia kikao cha Baraza la Wawakilishi hasa mawaziri kutoka chama hicho kwani nao ni miongoni mwa viongozi katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema kitendo
hicho cha wajumbe hao hasa mawaziri ni kitendo kibaya na ni
kumdhalilisha rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Alisema CCM kimeshangaa na hawakutarajia kitendo hicho kutokea hasa
ikizingatiwa kuwa CCM na CUF wamekubaliana na kuunda serikali ya umoja
wa kitaifa.
“Kilichotushtua ni mawaziri kutoka CUF kuungana na wajumbe wezao
kususia kikao kwa lengo la kukwamisha muswada wa sheria wa kuidhinisha
matumizi ya fedha za bajeti na kama mswada huo ungeshindwa kupitishwa
serikali ingeshindwa kufanya mambo yake ya msingi,” alisema Vuai.
Aliongeza: ”Kitendo kile sisi tunakiita ni vichekesho na vituko
kwani inaonyesha dhahiri yale mapenzi ya CCM kuungana nao na kupatikana
kwa SUK ili kuondokana na siasa za chuki na uhasama, wezetu tunaona
hawataki hivyo na sisi tutafikiria,” alisema. “Walichokifanya wezetu
hawa ni ubakaji wa kidemokrasia na unafiki wa kisiasa kwanini wasitoke
mwanzo wa vikao vya bajeti vilipoanza na kuamua kutoka ukingoni ambapo
zimebaki siku tatu tu rais kuvunja baraza hilo?” Vuai.
CHANZO:
NIPASHE
|
June 25, 2015
CCM YALAANI MAWAZIRI CUF KUTOKA BARAZANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment