![]() |
Fundi akisugua ukuta kabla ya kuanza kupaka rangi makao makuu ya CCM
mjini Dodoma jana ikiwa ni matayarisho kwa ajili ya vikao vya kamati ya
maadili, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho vitakavyo kaa
mapema mwezi ujao kwa ajili ya kuteua majina ya wagombea kuteuliwa
kugombea urais kupitia chama hicho. Picha na Edwin Mjwahuzi.
Dodoma. Kumekucha na Hapatoshi mjini Dodoma.
Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea hali ilivyo mjini hapa, wiki mbili
kabla ya vikao vya juu vya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuanza kazi ya
kumtafuta mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Hekaheka za maandalizi ya vikao hivyo kuanzia vya
maadili, Sekretarieti, Kamati Kuu, Halmashauri Kuu ya Taifa na Mkutano
Mkuu wa Taifa, zimeanza kuonekana wazi huku nyumba zote za kulala wageni
na hoteli zikiwa zimekwishajaa kwa muda wote wa vikao hivyo.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwenye maeneo ya
katikati ya mji wa Dodoma, umebaini kuwa nyumba za kulala wageni na
hoteli zimejaa kuanzia Julai 8 hadi 12, mwaka huu.
Hali hiyo imewafanya watu wanaotaka kupanga katika nyumba hizo kuulizwa wataondoka lini, ili tarehe za ‘booking’ zisigongane.
“Utaondoka lini, maana CCM wamechukua nyumba zote
hapa kati ya Julai 8 hadi 12,” alisema mmoja wa wahudumu katika nyumba
ya kulala wageni ya Kiramiya.
Chanzo cha habari kutoka katika ofisi ya CCM,
kimesema wajumbe wote 2,448 wa mkutano mkuu wamepata maeneo ya kulala
kwa siku watakazokuwa mjini hapa.
Hata hivyo, chanzo hicho kimedokeza kuwa
changamoto imekuwa katika kupata malazi ya wageni 600 waalikwa,
watakaokuja kuhudhuria mkutano mkuu huo utakaofanyika katika ukumbi mpya
wa chama hicho.
“Katika maeneo mengi tuliyokwenda tulikuta hoteli
zimechukuliwa na wapambe wa wagombea wa urais ambao tayari wamelipia
siku watakazokaa mjini hapa,” alisema mmoja wa wanakamati ya maandalizi
ya CCM na kuongeza:
“Hivi sasa wenzangu wako mtaani wanatafuta nyumba nyingine.”
Alisema hali imekuwa ngumu kutokana na wapambe wa
wagombea ambao hadi sasa wamefikia 39 kuchukua vyumba vingi na kuvilipia
kabisa, tofauti na CCM iliyopanga kuanza kulipia malazi hayo leo.
|
June 25, 2015
HAPATOSHI CCM DODOMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment