KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 27, 2015

CHENGE AGONGA MWAMBA ESCROW

Juhudi za mbunge wa Bariaadi Magharibi  Andrew Chenge ,(pichani),kutumia mkondo wa sheria kulizuia baraza la maadili  ya viongozi wa umma lisimuhoji kuhusu kuhusika kwake kwenye sakata la ESCROW ,zimegonga mwamba Mahakama kuu kutupilia mbali kesi aliyofungua kupinga hatua hiyo.Chenge alifungua kesi hiyo Mahakama kuu dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali  na sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma ,akipinga kuhojiwa dhidi ya tuhuma za kukiuka maadili ya viongozi baada ya kupokea Sh1.6 bilioni kutoka kwa mkurungezi wa VIP Engineering,James Rugemarila,fedha ambazo zinahusishwa na akaunti ya Tegeta ya Escrow .Washitakiwa katika kesi hio wawasilisha pingamizi la awali wakiiomba Mahakama ilitupilie mbali kesi hiyo pamoja na mambo mengine  wakidai imefunguliwa bila kufuata utaratibu wa kisheria .katika uamuzi wake jana ,Mahakama kuu ilikubaliana na hoja za pingamizi la awali za kutaka kutupilia mbali kesi hiyo uamuzi wake jana,Mahakama kuu ilikubaliana na hoja za pingamizi la awali za kutaka kutupilia mbali kesi hiyo uamuzi ambao unalipa Baraza la maadili fursa ya kuendelea na majukumu yake ya kumhoji Chenge dhidi ya tuhuma za ukiukwaji maadili ya umma. Mahakama kuu ilisema kuwa hoja za upande wa chenge,ulioongozwa na wakili Michael Ngalo ,hazina msingi

No comments:

Post a Comment