![]() |
| Prof.Mwandosya |
Akitoa taarifa ya kuondolewa kwa Muswada huo jana bungeni, Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Mark Mwandosya, alisema Muswada
huo ulichapishwa Februari 20, 2015 na kusomwa kwa mara ya kwanza bungeni
Machi 12, hadi Aprili Mosi, mwaka huu.
"Mheshimiwa Naibu Spika huu si muswada wa dharura kama ambavyo wengine wanazungumza,"alisema.
Alisema kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii,
iliyokutana Juni 22, mwaka huu ilijadili kwa kina Muswada huo na
kuzingatia maoni ya wadau wa tasnia hiyo na kushauri kuwa inahitaji muda
zaidi kuujadili na kuendelea kupata maoni zaidi ya wadau.
"Serikali imetafakari maoni ya kamati na kuafiki muswada uendelee
kufanyiwa kazi hadi hapo kamati itakapokamilisha kazi yake ipasavyo na
kuwakilisha maoni yake bungeni,"alisema.
Alisema matarajio ni kwamba muswada huo utasomwa kwa mara ya pili na ya tatu katika bunge lijalo.
Juni 22, mwaka huu, wadau mbalimbali wa habari, waliokutana mjini
Dar es Salaam walipinga muswada huo, kwa kile kinachoelezwa kuwa
unakiuka sheria za kimataifa, Katiba ya nchi na kuwanyima haki raia
kupata taarifa na kuua ndoto ya vijana wanaotarajia kunufaika na tasnia
ya habari.



No comments:
Post a Comment