KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 17, 2015

CHINA YAIPA TAKUKURU VIFAA VYA BILIONI 3/-

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah.                                                                   
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, imeikabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), vifaa vya kiufundi vya Sh. bilioni tatu kwa ajili ya kuiongezea ufanisi zaidi taasisi hiyo katika vita dhidi ya vitendo vya rushwa.
 
Vifaa hivyo vilikabidhiwa na Balozi wa China nchini, Dk. Lu Youqing, kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, na kushuhudiwa na watendaji wa taasisi hiyo katika ofisi zake za makao makuu jijini Dar es Salaam, jana.
 
Vifaa hivyo ni kompyuta za mezani 162 na mpakato 13,  printa za mtandao 20, skana 90, UPS 162, servers  4, SAN Storage moja, flashi 10 na simu ya mkononi moja, vyote vikiwa vya thamani ya Sh. bilioni tatu.
 
Dk. Hosea aliishukuru serikali ya China kwa msaada huo akisema vita dhidi ya rushwa inahitaji maamuzi ya haraka na matumizi ya vifaa vya kisasa ambavyo vina uwezo wa kukabiliana na wahusika wa vitendo hivyo.
 
Alisema kutolewa kwa vifaa hivyo ni uthibitisho dhahiri wa uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili na kuahidi kuvitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi katika kukabiliana na baadhi ya changamoto katika utekelezaji wa majukumu ndani ya taasisi hiyo.
 
Balozi  Youqing, alisema Tanzania na China, zimefurahia uhusiano baina yao kwa miongo mingi sasa katika maeneo mbalimbali yakiwamo ya kupambana na rushwa.

No comments:

Post a Comment