![]() |
| Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah.
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, imeikabidhi Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (Takukuru), vifaa vya kiufundi vya Sh. bilioni
tatu kwa ajili ya kuiongezea ufanisi zaidi taasisi hiyo katika vita
dhidi ya vitendo vya rushwa.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa na Balozi wa China nchini, Dk. Lu
Youqing, kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, na
kushuhudiwa na watendaji wa taasisi hiyo katika ofisi zake za makao
makuu jijini Dar es Salaam, jana.
Vifaa hivyo ni kompyuta za mezani 162 na mpakato 13, printa za
mtandao 20, skana 90, UPS 162, servers 4, SAN Storage moja, flashi 10
na simu ya mkononi moja, vyote vikiwa vya thamani ya Sh. bilioni tatu.
Dk. Hosea aliishukuru serikali ya China kwa msaada huo akisema vita
dhidi ya rushwa inahitaji maamuzi ya haraka na matumizi ya vifaa vya
kisasa ambavyo vina uwezo wa kukabiliana na wahusika wa vitendo hivyo.
Alisema kutolewa kwa vifaa hivyo ni uthibitisho dhahiri wa uhusiano
uliopo baina ya nchi hizo mbili na kuahidi kuvitumia kwa matumizi
yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi katika kukabiliana na
baadhi ya changamoto katika utekelezaji wa majukumu ndani ya taasisi
hiyo.
|
June 17, 2015
CHINA YAIPA TAKUKURU VIFAA VYA BILIONI 3/-
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment