![]() |
RAIS wa
Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameishukuru Serikali ya China kwa
kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya ikiwa
ni pamoja na kuendelea kuwaleta madaktari kila baada ya miaka miwili
hapa nchini.
Dk Shein
aliyasema hayo jana Ikulu mjini Zanzibar katika mazungumzo kati yake na
madaktari 25 kutoka China waliomaliza muda wao wa kazi nchini waliofika
Ikulu kwa ajili ya kumuaga Rais wakiongozwa na Balozi Mdogo wa nchi hiyo
anayefanya kazi zake Zanzibar, Xie Yunliang.
Katika
mazungumzo hayo, Dk Shein alisema utamaduni wa kuleta madaktari kutoka
China ni wa kihistoria ulioanzia mwaka 1965 na umeendelea kuwepo.
Dk Shein
alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wake wanathamini
na wanazipenda huduma mbalimbali zinazotolewa na madaktari hao.
Pamoja na
hayo, Dk Shein alitoa pongezi zake kwa Serikali ya China chini ya Rais
Xie Jingping kwa kuendelea kuisaidia Zanzibar katika miradi mbalimbali
ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba,
Ujenzi wa Uwanja wa Mao tse Tung na ujenzi wa jengo jipya la abiria
katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amaan Karume Zanzibar.
Kiongozi
wa madaktari hao 25, Dk Liu Yaping akitoa shukurani kwa niaba ya
madaktari hao alisema wamefurahia mazingira ya kufanyia kazi nchini na
ushirikiano walioupata kutoka kwa madaktari wazalendo wa Zanzibari kwa
ujumla.
(HABARI LEO)
|
June 17, 2015
DK SHEIN AISHUKURU CHINA KWA MISAADA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment