Kiongozi wsa Mbio za Mwenge
Kitaifa, Ndugu Juma Chum pamoja na mwezake wakiwatwisha ndoo za maji
Pelis Taolo na Jesca Msange wa Kijiji cha Kibedya muda mfupi baada ya
mradi wa maji wa Kibedya kufunguliwa.
………………………………………………………..
Na. Andrew Chimesela
Mwenge wa uhuru ambao kwa sasa uko
Mkoani Morogoro, umepitia miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mradi
wa maji uliogharimu shilingi 555,227,710.40 na unatazamiwa kuwapatia
maji safi na salama wananchi 10,534 ambao ni wakazi wa kijiji cha
Kibedya Wilayani Gairo.
Mwenge huo ambao umeingia siku yake ya pili, tangu kuwasili
Mkoani Morogoro ukitokea Mkoani Tanga, na kukimbizwa Wilaya ya Mvomero,
Leo ukiwa Wilayani Gairo umefungua mradi wa maji wenye matenki mawili
yenye jumla ya lita za ujazo 180,000.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa kwa Kiongozi wa mbio za
Mwenge Kitaifa Bw. Juma Khatib Chum, muda mfupi kabla kuufungua,
ilielezwa kuwa mradi wa maji wa Kibedya uliibuliwa na wananchi na
kuingizwa kwenye program ya Serikali ya miradi ya maji ya vijiji kumi
Wilayani Gairo.
Mradi wa Maji wa Kibedya umejengwa kwa ufadhili wa Benki ya
Dunia kupitia mpango wa maendeleo ya Sekta ya Maji, na wananchi
kuchangia ardhi ulipojengwa mradi huo yenye thamani ya shilingi
1,500,000,.00.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa lengo mahsusa la mradi huo ni
kuwapatia wananchi wa Kijiji cha Kibedya maji safi na salama hali
itakayochangia kuboresha maisha yao kwa kupata muda wa kutosha kufanya
shughuli nyingine za kiuchumi badala ya kutumia muda huo kutafuta maji.
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Juma Khatib Chum baada
ya kuufungua, mradi huo, aliwataka wananchi wa Kijiji cha kibedya
kuuendeleza na kuutunza mradi huo ili uweze kudumu kwa muda mrefu.
“ Ninawasihi wananchi wa Kijiji cha Kibedya kuendeleza na
kutunza miundombinu ya mradi huu pamoja na vyanzo vyake vya maji ili
mradi udumu kwa muda mrefu na kuja kunufaisha vizazi vingine vijavyo”
alisema.
Mwenge wa uhuru leo umekimbizwa katika Wilaya ya Gairo ambapo
umepitia jumla ya miradi ya maendeleo sita, yenye thamani ya shilingi,
905,071,355.40.
Hiyo ikiwa ni pamoja na mchanggo kutoka Serikali Kuu ni shilingi
715,390,635.40, mchango kutoka Halmashauri ya Gairo shilingi
7,578,720.00, nguvu za wananchi silingi 180,387,000.00 na wahisani
walichangia shilingi 1,715,000.00.
Mwenge wa Uhuru kesho utakimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. |
No comments:
Post a Comment