KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 12, 2015

HATIMAYE SERIKALI YASHUSHA KODI KWENYE MISHAHARA

mkuya Na Waandishi wetu, Dodoma/Dar
WAZIRI wa Fedha, Saada Mkuya Salum, amesema Serikali imeendelea na uboreshaji wa masilahi ya wafanyakazi ambapo kwa mwaka huu wa fedha imepunguza tozo la kodi ya mapato ya ajira kutoka asilimia 12 ya sasa hadi asilimia 11.
Akiwasilisha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2015/16 mjini Dodoma jana, Waziri Saada alisema hali hiyo inakwenda na dhamira ya Serikali kuwapunguzia mzigo wa kodi wafanyakazi.
Alisema mshahara wa kima cha chini umeongezeka kutoka Sh 65,000 mwaka 2005 hadi kufikia Sh 265,000 mwaka 2014/15, ambayo ni asilimia 307.7.
Waziri Saada, alisema Serikali imeendelea kufanya marekebisho ya Mfumo wa Kodi ya Mishahara (PAYE) kwa kupunguza kiwango cha chini kutoka asilimia 18.5 mwaka 2006/07 hadi asilimia 11 mwaka 2015/16 ikiwa ni punguzo la asilimia 35.
Katika kuhakikisha Serikali inawaangalia wafanyakazi wastaafu, alisema katika mwaka 2015/16, wataongeza kima cha chini cha pensheni kwa wastaafu wa Serikali kwa mwezi kutoka Sh 50,000 hadi Sh 85,000 sawa na ongezeko la asilimia 70.
“Serikali kwa kutambua mchango wa wazee wetu katika kujenga taifa hili, imedhamiria kuwalipa mafao ya kila mwezi, na kwa sasa Serikali imeanza kuandaa mfumo na utaratibu wa kuwatambua wazee wote nchini ili kupata idadi yao kamili na kuhakikisha mafao yanawafikia walengwa kwa wakati,” alisema. MTANZANIA

No comments:

Post a Comment