![]() | ||
| Dominique Strauss-Kahn
Mahakama MOJA nchini Ufaransa imemfutia kesi dhidi ya kujihusisha na makahaba nchini aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani Dominique Strauss-Kahn, Uingereza na Marekani.
Amekuwa akisisitiza kuwa hakuwa na taarifa kwamba wale wanawake aliokuwa akishirikiana nao katika kumbi mbalimbali za starehe katika nchi hizo walikuwa ni makahaba. Alikuwa anakabiliwa na kesi mbalimbali za kujihusisha na ukahaba katika sehemu mbalimbali za starehe nchini humo na kesi ilikuwa ianze kusiklizwa hivi punde. Ingawa ukahaba siyo kosa nchini Ufaransa kosa ni kuwaagiza kutoka maeneo mbalimbali ama kuwawezesha. Aliondolewa katika wadhifa huo kutokana na kujihuisha na vitendo mbalimbali vya kihuni ambavyo haviendani na hadhi yake ya Ukurugenzi katika IMF |
June 12, 2015
DOMINIQUE STRAUSS-KHAN AFUTIWA KESI UFARANSA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment