![]() |
| Baadhi ya akina mama na watoto wao wakisubiri watoto wao kupatiwa chanjo katika zahanati ya kijiji chaKashinga wilayani Ngara. |
![]() |
| Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua rasmi Chanjo ya watoto
kuzuia maambukizi ya magonjwa katika kata ya Nyakisasa kijiji cha
Kashinga akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ngara mkoani Kagera
lengo la ziara hiyo likiwani ni kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi
ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa chama, Katika ziara hiyo Kinana
anaongozana na Nape Nnauye na viongozi mbalimbali wa CCM kutoka mkoa wa
Kagera. Wanaoshuhudia tukio hili nyuma ni Mh. John Mongela Mkuu wa mkoa wa Kagera na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Mama Costansia Buhie. Wakati huo huo Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Ngara amesema Mamlaka ya Mapato TRA na Kikosi cha Usalama barabarani wana kila sababu ya kupeleka huduma zao utoaji wa leseni za udereva na huduma za usajiri wa vyombo vya moto mikoani na wilayani kwani ni usumbufu mkubwa wanaopata wananchi kufuata huduma hizo za Leseni za kuendesha vyombo vya moto na usajiri wa vyombo hivyo. Amezitaka taasisi hizo kufanya hivyo ili kuwaondolea wananchi usumbufu wanaoupata wanapohitaji huduma hizo kutokana na umbali, Wananchi wa Ngara wanalazimika kufuata huduma hiyo Bukoba mjini jambo ambalo linawaletea wananchi hao usumbufu mkubwa na upotevu wa fedha bila sababu ya msingi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NGARA) |




No comments:
Post a Comment