KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 16, 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AITIKISA CHATO MKOANI GEITA

1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasha mtambo wa maji uliojengwa Chato Mlimani kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji utakaohudumia wakazi wa mji huo leo wakati wa ziara yake katika mkoa wa Geita , Kinana anaendelea na ziara hiyo ya kikazi mkoani humo baada ya kumaliza ziara kama hiyo mkoani Kagera jana, Kinana anaendelea  na ziara hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015 na kuhimiza uhai wa chama, kukosoa na kutatua matatizo mbalimbali yanayokabili wananchi kwa maisha na maendeleo yao kwa ujumla akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSI CHA FULLSHANGWE-CHATO-GEITA)
2
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na Mkuu wa wilaya ya Chato Rodrick Mpogolo kulia wakipiga makofi mara baada ya kuwashwa rasmi kwa mtambo huo.                      
3
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Rodrick Mpogolo Mkuu wa wilaya ya Chato na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi pamoja na viongozi wa CCM wilaya ya Chato wakipunga mikono na wanaCCM mbalimbali katika picha ya pamoja.                     
5
Baadhi ya akina mama wakiwa na ndoo zao tayari kwa kuchota maji mara baada ya kuzindua rasmi mtambo wa maji Chato Kilimani ambao utahudumia wakazi wa mjini Chato na baadhi ya vijiji.                    

No comments:

Post a Comment