Afisa wa Jeshi la Magereza nchini, Nsajigwa Mwankenja akitoa maelezo kwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil kuhusu shughuli
zinazofanywa na Jeshi hilo, wakati Katibu Mkuu alipotembelea Banda la Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akipata
maelezo kutoka kwa Maafisa wa Uhamiaji kuhusu shughuli zinazofanywa na Idara hiyo,
wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maonyesho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akisoma
vipeperushi vya Idara ya Uhamiaji wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika
viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.


No comments:
Post a Comment