![]() |
RAIS Jakaya Kikwete
RAIS Jakaya Kikwete amekabidhiwa jumla ya magari ya kubebea wagonjwa
50 kutoka kwa kampuni ya vito ya Decent Dia Jewel (DMCC), yenye thamani
ya Dola za Marekani 300,000 kwa ajili ya kusambazwa maeneo mbalimbali
nchini.
Akizungumza baada ya kukabidhi funguo za magari hayo, Mwenyekiti wa
kampuni hiyo, Chetan Shah alisema magari hayo yatasafirishwa na kuwasili
rasmi nchini kuanzia mwezi Julai mwishoni hadi Agosti.
“Tunakukabidhi magari haya ya kubeba wagonjwa kwa ajili ya kusambazwa
maeneo mbalimbali, ikiwemo vijijini. Wazo la kutoa msaada huu
nililipata nilipotembelea Tanzania na kushuhudia namna wananchi hasa wa
vijijini walivyokuwa wakitaabika kwa kukosa huduma za afya kutokana na
ukosefu wa usafiri,” alisema Shah.
Alisema amekuwa akitembelea Tanzania mara kwa mara hasa kutokana na
biashara ya kampuni yake ya madini na ndipo alipopata uamuzi wa kutoa
magari hayo kusaidia wale wote wasio na uwezo wa usafiri katika sekta ya
afya.
Kwa upande wake, Rais Kikwete aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo
na kukiri kuwa bado kuna maeneo nchini yenye uhitaji mkubwa wa magari
ya wagonjwa. “Hili ni eneo ambalo ki ukweli bado lina uhitaji mkubwa.
Tunashukuru sana kwa kufikiria kutusaidia na kwa kweli msaada huu utatufaa sana,” alisema.CHANZO HABARI LEO
|
June 19, 2015
KIKWETE AKABIDHIWA MAGARI 50 YA WAGONJWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment