![]() |
Zanzibar.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wamemzuia Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kuhudhuria shughuli ya kuvunja
Baraza hilo itakayoongozwa na Rais Dk Ali Mohamed Shein leo.
Uamuzi
huo ulitolewa baada ya Spika wa Baraza hilo, Pandu Ameir Kificho kutoa
utangulizi kwa wajumbe akiwataka watengue kanuni ili viongozi wa kitaifa
watakaohudhuria shughuli hiyo waweze kuingia ukumbini badala ya kukaa
sehemu ya kawaida ya wageni waalikwa.
Baada ya
kutoa utangulizi, Spika Kificho alianza kuwahoji wajumbe wanaokubali
viongozi wa kitaifa waruhusiwe kuingia ndani ya Ukumbi wa Baraza kwa
kuwataja wakiwamo Rais wa Zanzibar, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman
Makungu, mpambe wa Rais na kuungwa mkono kwa kupigiwa makofi na sauti za
ndiyo.
Hata
hivyo, alipomtaja Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad
wajumbe wote waliokuwapo katika Baraza hilo, ambao wote ni wa CCM,
walikataa wakisema kwa sauti “hapana,” kitendo ambacho kilimfanya Spika
kurudia kutamka jina hilo kwa zaidi ya mara tatu na majibu yalikuwa
hapana.
Hatua ya
wawakilishi kumkataa Maalim Seif, imekuja siku moja baada ya mawaziri na
wajumbe wa CUF kutoka nje ya Baraza wakisusa kujadili na kupitisha
muswada wa sheria wa bajeti kuu ya matumizi ya Serikali ya mwaka wa
fedha 2015/16 wakipinga pamoja na mambo mengine, mchakato unaoendelea
sasa wa uandikishaji wapigakura katika Daftari la Kudumu.
“Mnakubali
kutengua kanuni kuruhusu viongozi wa kitaifa kuhudhuria katika shughuli
yetu ndani ya ukumbi? Wageni wetu ni Rais wa Zanzibar, mpambe wake,
Jaji Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais,” alihoji Spika Kificho lakini
alipingwa baada ya kulitaja jina la Makamu wa Kwanza wa Rais.
Awali,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed
aliwasilisha hati ya Serikali kuhusu marekebisho ya kanuni za Baraza.
Waziri
Aboud alisema, Rais wa Zanzibar atakagua gwaride maalumu la Polisi kabla
ya kuhutubia Baraza hilo saa 9.30 alasiri na kuwataka wajumbe wote
kufika kabla ya kuwasili kwa Rais.
Kuhusu
uamuzi wa kumkataa Maalim Seif, Aboud alisema upo katika mamlaka ya
wajumbe kwa mujibu wa kanuni za Baraza hilo na kwamba hatua itakayofuata
ni Spika kumwandikia barua Maalim Seif ya kutohudhuria shughuli hiyo
ili kulinda uamuzi wa baraza hilo |
June 27, 2015
MAALIM SEIF AZUIWA KUINGIA BARAZA LA WAWAKILISHI LIKIVUNJWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment