| kulia ni Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi akipokea mkataba wa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo,Jackson Mayanja mara baada ya kuusaini leo ambapo amesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo,katika Halfa iliyofanyika mjini hapa,Picha kwa Hisani ya Coastal Union. |
| Kocha Mkuu mpya wa timu ya Coastal Union,Jackson Mayanja kushoto akisaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo kulia ni Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi,Picha kwa Hisani ya Coastal Union. |
| Kocha Mkuu mpya wa timu ya Coastal Union,Jackson Mayanja kushoto
akisaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo kulia ni Katibu Mkuu wa
Coastal Union,Kassim El Siagi,Picha kwa Hisani ya Coastal Union.
Akizungumza
baada ya kumalizika zoezi hilo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema
kuwa kutokana na umahiri aliokuwa nao kocha huyo wanaimani kubwa ataipa
mafanikio timu hiyo hasa katika harakati za kuhakikisha inafanya vizuri ligi
kuu msimu ujao.
Amesema kuwa
uwezo wa Kocha huyo utaleta matumaini makubwa ya mafanikio hasa ukizingatia ni
kocha mwenye uwezo mzuri wa kufundisha na kuzipa mafanikio timu hivyo tunaamini
kuja wake kwetu itakuwa chachu katika maendeleo.
Mayanja
ambaye aliwahi kuzifundisha timu za soka Kiyuvu FC ya Rwanda,Timu ya Mamlaka ya
Mapato nchini Uganda (URA),Vipers FC ya
Bunamwaya na KCC ya Uganda amesema kutua
kwenye timu hiyo kumpa faraja kubwa hivyo atahakikisha anatoa mchango wake
kwenye kuipa mafanikio.
Amesema kuwa
mipango yake mikubwa ni kuhakikisha timu hiyo inang’ara katika michuano ya Ligi
kuu msimu ujao ikiwemo kubadili aina ya mchezo wa timu hiyo ili iweze kupata
mafanikio kwa kuweka umoja baina ya wachezaji mashabiki, wanachama na wapenzi.
Amesistiza
pia umuhimu wa mshikamano baina ya wapenzi,wanachama na viongozi ili kuiwezesha
timu hiyo kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao kwani dhamira yake ni kutaka
kuona timu hiyo inang’ara kwenye medani za kitaifa na kimataifa.
Mwisho.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO CHA COASTAL UNION.
|


No comments:
Post a Comment