KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 24, 2015

MBUNGE WA GEITA, DONALD MAX KUZIKWA JUMAMOSI

Akitangaza taarifa za msiba huo, mapema leo asubuhi bungeni mjini Dodoma, Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema wamepokea taarifa hizo kwa masikitiko, ambapo mbunge huyo alifariki jana katika HospitalI ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa muda mrefu.
Spika Makinda amesema taarifa za awali zinasema mwili wa marehemu utazikwa siku ya Jumamosi jijini Dar lakini bado anaendelea kuwasiliana na familia ya marehemu.
Kufuatia msiba huo, Spika ameliahirisha bunge mpaka kesho saa 3 asubuhi.
Mungu ailaze roho ya marehemu, mahali pema peponi, AMEN.

No comments:

Post a Comment