![]() |
| Marehemu Donald Max, aliyekuwaMbunge wa Geita (CCM) Dodoma. Mbunge wa Geita (CCM), Donald Max (58) amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kuwa mbunge huyo (pichani) alifariki jana saa 12.00 jioni katika hospitali hiyo.
Ndugai alisema Max alikuwa mahututi kwa kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita.
“Taratibu za maandalizi ya mazishi kwa sasa bado maana ni kama dakika 15 zilizopita ndiyo kafariki,” alisema Ndugai.
Max alizaliwa Mei 22 mwaka 1957 na kusoma katika
Shule ya Msingi ya Salvatorian Convent na baadaye kujiunga na Shule ya
Sekondari ya Azania mwaka 1971 hadi mwaka 1974.
Mwaka 1980 alikwenda nchini Urusi na kusoma kozi
ya ufundi katika Chuo cha Ufundi cha Roston on Don kabla ya kujiunga na
Taasisi ya Volgograd Polytechnical nchini humo na kutunukiwa Shahada ya
Uzamili katika Uhandisi.
|
June 24, 2015
MBUNGE WA GEITA AFARIKI DUNIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment