KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 25, 2015

MGOMBEA URAIS CCM ADUWAZWA.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe.                                                                        
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Boniface Ndengo (40), amesema  mchakato wa kusaka wadhamini mikoani umegubikwa rushwa na kumweka katika mazingira magumu kupata wa wadhamini kwenye baadhi ya maeneo nchini.
 
Ndengo alitoa kauli hiyo jana baada ya kurejesha fomu ya kugombea urais kwenye makao makuu ya CCM mkoani Dodoma.
 
Alisema kuna wanachama katika baadhi ya mikoa nchini waligoma kumdhamini kwa madai kuwa hagawi fedha kama walikvyokuwa wakifanya makada wengine wa chama hicho.
 
Kada huyo aliyekuwa amefuatana na wanawe wanne na mkewe, aliutaja mkoa mmojawapo uliomfedhehesha kutokana na kutakiwa atoe fedha kwa wanachama ndipo adhaminiwe kuwa ni Kagera.
 
Ndego ambaye ni mjasiriamali kutoka kijiji cha Mjimtala, Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, alijitosa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama chake kugombea urais Juni 11, mwaka huu.
 
 Mgombea huyo alirejesha fomu hiyo jana makao makuu ya CCM Dodoma saa 8:13 mchana na kumkabidhi Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Oganaizesheni, Muhammad Seif Khatibu.
 
“Changamoto nilizokutana nazo huko mikoani nilikopita zinanipa shaka kubwa kutokana na zao la rushwa ambalo kwenye baadhi ya mikoa nilikosa wadhamini. Wanachama walinieleza hawawezi kunidhamini kama sitawapa fedha…waliniuliza mbona wenzako waliokuja walitupa fedha, wewe hutupi?,” alisema Ndengo.
 
Hata hivyo,  alisema amezunguka katika mikoa 12 nchini ikiwamo mitatu ya Zanzibar na kupata wadhamini 612.
 
Kufuatia changamoto hiyo, Ndengo alisema CCM inapaswa kuwa makini wakati wa kumtafuta mgombea wa urais atakayepeperusha bendera katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu na kuonya kuwa  ikifanya makosa ya uteuzi, kiongozi atakayepatikana atakuwa ni zao la rushwa.

2 comments:

  1. Kumbukumbu hii itunze isopotee maana miaka ijayo itatafutwa!

    ReplyDelete
  2. Vipaumbele vya Mh. Boniface Ndengo ni pamoja na kuifanya Tanzania kuwa Lango kuu la biashara kwa nchi za Afrika na Kituo cha Utalii barani Afrika

    ReplyDelete