Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amezima
mgogoro ndani ya magazeti ya Uhuru na Mzalendo yanayomilikiwa na chama
hicho kupitia kampuni ya Uhuru Publications.
Hatua hiyo ilifikiwa jana jijini Dar es Salaam baada ya Nape kufanya mazungumzo na wafanyakazi hao.
Wafanyakazi wa magazeti hayo walishiriki mgogoro huo uliohusishwa
na masuala ya siasa, chanzo chake kikitajwa kuwa ni hatua ya Bodi ya
kampuni ya Uhuru Publications kufanya mabadiliko ya uongozi wake na
kumbadilishia kazi Mhariri Mtendaji wake, Joseph Kulangwa.
Nape alimthibitishia mwandishi wetu kushiriki kwake kikao na
wafanyakazi wa kampuni hiyo, huku akisisitiza kuwa baada ya mazungumzo,
pande zote zilielewana na mgogoro huo kumalizika.
Hatua zilizofikiwa na bodi ya kampuni hiyo, licha ya kumbadilishia
kazi Kulangwa, iliwabadilisha kazi watendaji wengine watatu wa idara ya
biashara, ukaguzi na rasilimali watu kuanzia Jumanne iliyopita.
Taarifa za ndani zilieleza kuwa Kulangwa ambaye awali alikuwa
mwajiriwa wa magazeti ya Tanzania Standard Newspapers (TSN)
inayomilikiwa na serikali, alishika wadhifa huo miezi 13 iliyopita.
Kuhusu mtikisiko wa kiuchumi ulioikabili kampuni hiyo, inaelezwa
kuwa sekretatieti ya CCM chini ya Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana, ilitoa
zaidi ya Shilingi milioni 400 katika kulipa madeni ikiwamo uchapaji na
ulipaji mishahara kwa wafanyakazi wa Uhuru.
CHANZO:
NIPASHE



No comments:
Post a Comment