Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Ruangwa Bw. Nicholous Kombe akimsikiliza Meneja wa Huduma
kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akimshukuru kwa Halmashauri hiyo
kusaidia kikundi cha vijana kwa kuwawezesha fedha na udongo kwa ajili ya
kutengeneza matofaliya kufungamana. Katikati ni Meneja wa NHC Mkoa wa
Lindi Bw. Mussa Patrick Kamendu.
Jengo la Ofisi ya kikundi cha
vijana cha Narunye(hakuna kutegeana) katika Halmashauri ya Wilaya ya
Lindi Vijijini likiwa limeonwa na Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru
kama inavyoonekana. Kikundi hiki kimeshaanza kupata maombi mengi ya
matofali kutoka kwa wananchi wanaohitaji.
Kikundi cha vijana cha Ruangwa
Materials Group katika Halmashauri ya Wilaya Ruangwa kimeshatengeneza
matrofali kwa kutumia mashine ya msaada kutoka NHC. Halmashauri ya
Wilaya hiyo imeamua kuyatumia matofali ya vijana hawa kujengea zahanati
na majengo mengine yanayohitajika katika Halmashauri zikiwemo nyumba za
Waalimu.
Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi Bw.
Mussa Patrick Kamendu akitoa mawaidha kwa kikundi cha vijana cha Narunye
kilichopo katika Wilaya ya Lindi vijijini baada ya kutembelea kikundi
hicho kukagua kazi zake.Vijana hawa wanajihusisha pia na utunzaji
mazingira.






No comments:
Post a Comment