![]() |
Dr Kalokola
Tanga. Jeshi la Polisi limesema
lipo katika hatua za mwisho za kukamilisha upelelezi wa tukio la askari
wa CCM kumshambulia mtangazania ya urais kupitia chama hicho, Dk
Muzzammil Kalokola.
Dk Kalokola alishambuliwa na askari hao , maarufu
kwa jina la Green Guard, Juni 17 wakati alipotaka apewe kipaza sauti ili
aombe wadhamini kwenye mkutano ambao uliandaliwa kwa ajili ya
kumdhamini mgombea mwingine wa urais kwa tiketi ya chama hicho, Edward
Lowassa.
Picha za video zilizosambaa kwenye mitandao
mbalimbali ya kijamii zinawaonyesha askari hao wakimburuza na baadaye
kumpiga ngwala iliyomuangusha chini na mkoba wake ulio na fomu za
kuwania urais ukiwa chini.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Zubery
Mwombeji alisema jeshi hilo likikamilisha upelelezi litapeleka jalada
kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili aweze kutafsiri nguvu iliyotumika
kumshambulia na kama waliohusika wanastahili kufikishwa mahakamani.
Mwombeji alitoa taarifa hiyo jana alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua ambazo jeshi hilo
limechukua baada ya tukio hilo.
“Tupo katika hatua za mwisho za upelelezi wa tukio
la kushambuliwa kwa mtangazania wa CCM. Mwanasheria wa Serikali ndiye
mwenye mamlaka kisheria ya kutafsiri na ndiye pia mwenye jukumu la
kuamua nini kifanyike,” alisema Mwombeji.
Aliwataja watu wanne wanaopelelezwa kutokana na
kuhusishwa na tukio hilo, akiwamo kiongozi wa kundi la vijana wa CCM
wanaojulikana kwa jina la Greenguard na mmoja wa makatibu wa CCM
wilayani Tanga ambao majina yao tumesitiri kwa sasa.
Dk Kalokola alishambuliwa wakati alipokuwa akitaka
ashughulikiwe kwanza kabla ya mgombea aliyeandaliwa mkutano huo kufika,
akidai kuwa ana masuala yanayombana na hasa kesi aliyoifungua ya
kupinga mchakato wa Katiba.
Kada huyo alijitetea kuwa alikuwa na miadi na katibu wa CCM siku hiyo na alikuwa anapita kwenye eneo la mkutano.
Dk Kalokola alikiri kupigwa katika tukio hilo
lilitokea mchana Jumatano ya Juni 17, 2015 alipofika kwenye ofisi za CCM
za Wilaya ya Tanga Mjini.
“Tulielekezwa kuwa makatibu wa CCM wa mikoa ndiyo
watakaotutafutia wadhamini siyo sisi tutafute hivyo mimi tarehe 16
nilikwenda ofisi za CCM kuripoti kwa katibu wa Mkoa,” alisema.
Hata hivyo, alisema hakuweza kuonana na katibu
huyo baada ya kuambiwa kuwa hayupo na amemwachia majukumu hayo katibu wa
CCM wa Wilaya ya Tanga Mjini.
|
June 23, 2015
POLISI YACHUNGUZA WANNE WALIOMPIGA MGOMBEA URAIS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment