![]() |
| Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujenga utamaduni mpya wa kukubali matokeo na kumuunga mkono mgombea anayeteuliwa na chama hicho kugombea nafasi ya Urais mwaka huu badala ya kujenga na kuendeleza makundi yanayoweza kuvuruga umoja na kuhatarisha mustakabali mzima wa chama hicho.
Pinda ambaye ni miongoni mwa zaidi ya wanachama 30 wa chama hicho
waliochukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais kupitia CCM mwaka
huu, aliyasema hayo jana jijini Mbeya alipokuwa akitafuta wadhamini.
Alisema kuwa ingawa watu waliojitokeza kuchukua fomu za kuomba
kuteuliwa na CCM kugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka
huu ni wengi, lakini anayetafutwa ni mmoja, hivyo haiwezekani wote
waliochukua fomu hizo kufanikiwa kupata nafasi ya kuteuliwa kugombea
urais kupitia CCM.
“Nitoe rai kwa wadau wote, ni kwamba ilimradi sisi wote tuliomo
humu ni wana-CCM, na wote waliojitokeza kugombea nafasi hii ni wana-CCM,
lazima tujenge tabia, tujenge mwenendo mzuri wa kuona namna gani huyo
moja atakayepatikana wengine wote tuliokuwa kwenye mchakato huo turudi
tumuunge mkono maana ndiye atakuwa mgombea wetu aliyepatikana,” alisema
Pinda na kuongeza:
“Ifahamike kuwa hata kama tungekuwa watu mia tuliochukua fomu,
anayetafutwa ni mmoja tu, haiwezekani sote sisi tukang’ang’ania
tuteuliwe, hivyo katika mazingira haya ni muhimu tujenge utamaduni mpya
wa kuridhika na uteuzi kisha tumuunge mkono huyo atakayeteuliwa,”
alisema Pinda.
Aidha aliwataka wagombea wenzake kutonuna baada ya uteuzi kufanyika
na badala yake wavunje makundi yao na kumuunga mkono mtu atakayeteuliwa
kwa manufaa na maslahi ya chama na Watanzania kwa ujumla.
Pinda lisema kuwa endapo wagombea wote kila mmoja atang’ang’ania
ateuliwe huku wakiendeleza makundi na kupigana vijembe hata baada ya mtu
anayetafutwa kupatikana, ni dhahiri kuwa CCM itayumba na pengine
kudhoofika.
CHANZO:
NIPASHE
|
June 18, 2015
PINDA: TUSIPOTEULIWA TUYAKUBALI MATOKEO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment