![]() |
| Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Shaaban Issa Simba Viongozi wa makundi mbalimbali ya jamii wamemlilia Mufti Shaaban Issa Simba, aliyefariki dunia jijini Dar es Salaam jana huku wakimmwagia sifa mbalimbali.
Mufti Simba alifariki dunia jana asubuhi katika hospitali ya TMJ ya
jijini Dar es Salaam alikokuwa anatibiwa maradhi ya kisukari na
shinikizo la damu.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim,
alithibitisha kutokea kwa kifo hicho kilichotokea saa 1:00 asubuhi.
“Ni kweli Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Shaaban Issa Simba,
amefariki hii leo (jana) asubuhi kwa maradhi ya kisukari na presha,”
alisema kwa ufupi Sheikh Alhadi.
Alisema msiba huo siyo msiba wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) peke yao, bali pia ni kwa Waislamu wote Tanzania.
Alisema mwili wa marehemu utapelekwa leo Bakwata majira ya asubuhi na kufanyiwa sala, mawaidha na sala.
Aliongeza kuwa majira ya mchana mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea Mkoa wa Shinyanga na anatarajiwa kuzikwa keshokutwa.
“Asubuhi kesho (leo), Waislamu wote wanahitajika kufika Bakwata
makao makuu ambapo taratibu zitaendelea hapa, na mengi yataelezwa hapa
na viongozi wengi wa kitaifa watakuwapo,” alisema Sheikh Mussa.
Aliongeza kuwa Mufti alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya sukari na
presha kwa muda mrefu na hivi karibuni alikuwa amesafiri na aliporudi
mapafu yake yalikuwa na tatizo lilisababisha kupumua kwa taabu.
Alisema mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo.
JK ATUMA SALAMU
Rais Jakaya Kikwete, ametuma salamu za rambirambi kwa Waislamu wote nchini na Bakwata kufuatia kifo cha Mufti Simba.
“Kifo kinaleta huzuni, hata hivyo kifo hakizuiliki, hatuna budi
kukikubali na ni wajibu wetu kumuombea Sheikh Mkuu kwa Mola wetu ampe
mapumziko ya milele,” Rais Kikwete alisema katika salamu hizo kupitia
kwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum.
"Nawaombea subira wana familia, ndugu, jamaa, Waislamu wote na wana
jamii kwani Mufti alikua kiongozi katika Jamii yetu,'” Rais alisema na
kuongeza:
“Kamwe mchango wake hautasahaulika katika jamii yote kwa ujumla na hakika sote tutamkumbuka.”
Rais alimuelezea Marehemu Mufti kama mwalimu katika jamii ambaye
alikuwa na uzoefu wa hali ya juu na mwenye kupenda dini yake na kuitumia
kwa manufaa ya jamii iliyomzunguka
“Amekuwa mwalimu imara na mtu wa kutumainiwa na kutegemewa katika
Uislamu na jamii kwa ujumla, hakika tutamkumbuka siku zote,” Rais
Kikwete aliongeza.
|
June 16, 2015
RAMBIRAMBI SHEIKH MKUU KILA KONA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment