KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 24, 2015

RWANDA :KUKAMATWA KWA KACHERO WETU NI UPUUZI MTUPU

   Rwanda imelichukulia tukio la kukamatwa kwa kachero wake mkuu Karenzi Karake kuwa ni 'upuuzi'Jen. Karake, 54, alikamatwa katika uwanja wa ndege wa |Jumamosi iliyopita,akituhumuwa kuamrisha mauaji , kuelekea mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Alikamatwa na Polisi wa Uingereza kupitia hati ya Umoja wa Ulaya kwa niaba ya serikali ya Uhispania,Williams Nkurunziza, Balozi wa Rwanda nchini Uingereza liliita tukio hilo kama uchokozi.

Msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alisema lilikuwa ni suala la 'msako'zaidi na kwamba polisi walikuwa na haki za kumkamata chini ya hati ya Umoja wa Ulaya.
 
Louise Mushikiwabo, Waziri wa Mambo ya nje wa Rwanda, aliuita ukamataji huo kama upuuzi : "Mshikamano wa Ulaya na Afrika ni wa kinafiki,"alisema

Mwaka 2008,Jaji Mpelelezi wa Uhispani, Andreu Merelles alimfungulia mashitaka  Jen.Karake na wengine 39 ambao wako jeshini au walishatoka kwa madai ya mauaji.

Anatuhumiwa kwa kuamrisha mauaji ya mwaka 1997 ya raia watatu wa Uhispania waliokuwa wakifanya kazi na shirika lisilo la kiserikali la Medicos del Mundo.

Lakini Rwanda inasema kwamba jambo hilo ni kitendawili kwani amekuwa akisafiri sana kwenda Uingereza tangu hati hiyo itolewe.

Balozi Nkurunziza aliiambia wa BBC kuwa wanatafakari madai hayo ya mauaji ya kimbari.


"Tuhuma kwamba viongozi wetu arobaini wana hatia ya kuvunja haki za kibinadamu ni uchokozi

Jen Karake yuko rumande atafikishwa mahakamani leo na kesho.

Msemaji wa mahakama kuu ya Uhispania amesema Uingereza ndio yenye mamlaka ya kuamua iwapo apelekwe Uhispnia au la.

No comments:

Post a Comment