![]() |
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein
leo anatarajiwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya
urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini
hapa.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri
Kuu, Itikadi na Uenezi ya CCM Zanzibar Waride Bakari Jabu, Dk Shein
ambaye ni Rais wa Zanzibar atakabidhiwa fomu ya urais na Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Waride
alisema mara baada ya Dk Shein kukabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya
kuwania nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM, atazungumza na viongozi wa
chama hicho wakiwemo wa wilaya na mikoa ya Unguja na Pemba.
Baadhi ya
viongozi ambao atapata nafasi ya kuzungumza nao ni pamoja na wazee wa
chama na waasisi wa mikoa mitatu ya Unguja na Pemba.
DK Shein
anakuwa mgombea wa kwanza wa CCM kuchukua fomu kuwania nafasi ya urais
wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho, ingawa kwa upande wa upinzani,
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad ambaye pia ni Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameshachukua fomu.
Wawili
hao walichuana katika uchaguzi mkuu uliopita na Dk Shein kutangazwa
mshindi, lakini baadaye iliundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Taarifa
ya chama hicho imesema kwamba hadi sasa hakuna jina la mwanachama wa CCM
aliyetangaza nia ya kutaka kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo ya juu ya
uongozi kwa Chama Cha Mapinduzi.(HABARI LEO)
|
June 18, 2015
SHEIN KUCHUKUA FOMU YA URAIS ZANZIBAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment