i. Wizara ya Maliasili na Utalii
inashiriki kwenye Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dares
Salaam (Saba Saba) yatakayofanyika katika viwanja vya Mwalimu
Julius.K.Nyerere, Barabara ya Kilwa kuanzia tarehe 28 Juni hadi 8 Julai,
2015.
ii. Karibu kwenye Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ujionee
na kuelimika kuhusu shughuli za Utalii, Ufugaji Nyuki, Uhifadhi wa
Misitu, Malikale na Wanyamapori.
iii. Safari za kutembelea Hifadhi za Mikumi na Saadani kwa gharama nafuu zitakuwepo
iv. Aidha, Wizara itachezesha bahati nasibu ambapo mshindi atazawadiwa safari ya kwenda kutembelea Hifadhi ya Mikumi au Saadani.
v. Pia, Utapata fursa ya kuwaona wanyamapori hai kama vile Chui,
Mamba, Nyoka, Ndege wa aina mbalimbali pamoja na mfalme wa pori SIMBA.
“Unganisha Uzalishaji na Masoko ”



No comments:
Post a Comment