Watu 200 wamekusanyika nje ya ubalozi wa Uingerenza jijini Kigali nchini Rwanda kupinga kukamatwa kwa Jen Karenzi Karake nchini Uingereza
Waandamanaji wametishia kutosimamisha maandamano nje ya ubalozi katika mji mkuu wa Kigali hadi atakapo hachiwa huru,atafikishwa kortini leo.
Serikali ya Rwanda imechukulia kukamatwa kwake kama" upuuzi"Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amelaumu kushikiliwa kwa Jen Karake na kusema kuwa "mshikamano wa ulaya kuikandamiza Afrika haukubaliki
Mwakilishi wa BBC Afrika mashariki Karen Allen anasema kuwa kauli ya waziri huyo imechochea maandamano hayo ya jana
"Tuko hapa tukishikamana na mashuja wetu ambao walikuwa miongoni mwa waliosimamisha mauaji ya kimbari nhini mwetu,'' anasema Herbert Muhire,mmoja wa waandamaji
Balozi wa Uingereza nchini Rwanda ,William Gelling, kwa ufupi aliwahutubia waandamanaji na kusema;
"Naweza kusema kuwa haya ni maamuzi ya sahihi ya kisheria kama mnavyoelewa ...Uingereza ni mshirika wa karibu wa Rwanda


No comments:
Post a Comment