![]() |
| UTII WA SHERIA BILA SHURUTI” Msanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi anayeshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, Jesca Kindole (Safina) akilipigia saluti sanamu la askari wa Jeshi la Polisi wa kipindi cha kikoloni, wakati msanii huyo na wenzake walipotembelea mabanda ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. |
![]() |
| Wasanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi wanaoshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, wakipewa maelezo na Koplo wa Jeshi la Polisi, Sylvester Mganga, kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Jeshi hilo, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Habib Mrisho (Sumaku), Jesca Kindole (Safina) na Rashid Costa (Maringo 7). |




No comments:
Post a Comment