KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 12, 2015

WATOA HUDUMA MKOANI LINDI WAASWA KUCHANGAMKIA MIKOPO INAYOTOLEWA NA NHIF ILI KUBORESHA HUDUMA ZA MATIBABU-RAS LINDI

3
Meneja wa Mfuko Mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akifafanua dhamira ya mfuko katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya afya,kupitia mikopo iliyoboreshwa ,kwani hadi kufikia mwezi mei.2015 watoa huduma wa mkoa wa Lindi wameweza kukopa takribani 135mil.ambapo kati ya fedha hizo hospitali ya mkoa ilikopa ultra sound yenye thamani ya 54Mil.amesisitiza kuwa huduma zinapoimarika  hususani upatikanaji wa dawa wananchi hawatasisita kuchangia kwenye CHF.
4
Mtoa elimu afisa kutoka makao makuu ya mfuko isaya shekifu akiwasilisha mada inayotoa miongozo na taratibu za maombi ya mikopo,ambapo aliwataka watoa maamuzi kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za matibabu kwani kutachochea wananchi wengi kujiunga na CHF, hivyo kuongeza mapato ya hospitali,kwa sasa mfuko umetenga jumla ya 2bilioni ili watoa huduma wa serikali,binafsi na mashirika ya dini waweze kukopa.  
5
Mganga mfawidhi kituo cha afya mjini kati Lindi Dr. Zulfa Msami akiuliza jambo baada ya uwasilishwaji wa mada                     

No comments:

Post a Comment