…………………………………………………..
Wakulima na wageni mbalimbali
watakaoshiriki kwenye maonesho ya nanenane ya mwaka huu wanatarajia
kupata punguzo la bei ya simu za smartphones kutoka Tigo katika jitihada
za kampuni ya mawasiliano ya simu kuwapatia watanzania wengi
iwezekanavyo kupata kufurahia mambo ya kimtandao.
Akitangaza ushiriki wa Tigo
katika maonesho ya nanenane ya mwaka huu kwenye mkutano na waandishi
wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, meneja mawasiliano wa
Tigo Bw. John Wanyancha alisema, gharama nafuu za smartphones ni sehemu
ya lengo la kampuni la kukuza mabadiliko ya maisha ya kidijitali kwa
kuwapa watanzania upatikanaji wa mtandao wa intaneti kupitia simu zao
za mkononi.
Lengo letu ni kuwafanya watu
waujue ulimwengu, ulimwengu ambao una fursa za kijamii na kiuchumi
zisizokuwa na kikomo. Tunawahimiza wageni watakaotembelea maonesho ya
nanenane kupita kwenye banda la Tigo ili kujionea bidhaa zetu mbalimbali
za kidijitali na zenye umuhimu zaidi, “tembea na simu ya smartphone
iliyounganishwa na intaneti kwa bei yenye punguzo, ” alisema Wanyancha.
Bidhaa nyingine zitaonyeshwa na
kampuni siku ya nanenane, ambayo mwaka huu itafanyika kitaifa mkoani
Lindi, bidhaa hizo ni pamoja na Tigo Kilimo – Huduma inayolenga kukidhi
mahitaji ya wakulima kwa kuwapa taarifa kuhusu upatikanaji wa mbolea,
soko la mazao yao na utabiri wa hali ya hewa.
Kampuni ya Tigo ndiyo
mdhamini mkuu wa maonesho ya nanenane mwaka huu.
Tunawahimiza wakulima katika
mikoa ya kusini ya Mtwara, Lindi na Pwani kutembelea banda letu na
kujifunza juu ya jinsi ya kupata taarifa muhimu kwa urahisi kuhusu
kilimo kupitia simu za mkononi,” alisema Wanyancha na kubainisha kuwa
Tigo Kilimo pia inapatikana kupitia vipengele vya kwenye simu.
Mkutano wa waandishi wa habari ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa shirika la Tanzania Agricultural Society (TASO)
Engelbert Moyo ambaye alisema kuwa, maonesho ya nanenane ya mwaka huu
yatavutia washiriki kutoka sekta ya mawasiliano ya simu, madini,
kusindika mazao, nishati, misitu, utalii, mifugo na sekta ya nyuki.
Taasisi zote muhimu za serikali
pia zitashiriki maonesho ikiwa ni pamoja na wizara ya Kilimo chakula na
Ushirika,Viwanda na Biashara, Maliasili na Utalii; Nishati na Madini,
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,Mambo ya Ndani, ulinzi, miongoni mwa
wengine kama kawaida.
"Tunatarajia viongozi wakubwa wa serikali kutembelea
maonesho ikiwa ni pamoja na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein
ambaye ndiye amepangwa kufungua rasmi maonesho ya nanenane mwaka huu," alisema Moyo.
No comments:
Post a Comment