KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 1, 2015

Kiungo mahiri anayekuja kwa kwa kasi ndani ya Yanga, Geofrey Mwashiuya.
Said Ally na Saphyna Mlawa
KIUNGO mahiri anayekuja kwa kwa kasi ndani ya Yanga, Geofrey Mwashiuya amechukua maamuzi magumu magumu ndani ya klabu hiyo kwa kuikataa jezi namba 19 aliyopewa na uongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kuitumia katika msimu ujao.
Kiungo huyo ambaye jana alipewa mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo alisema hataki kuvaa jezi hiyo bali anataka namba kumi.
Mwashiuya ameikataa jezi hiyo namba 19 iliyokuwa inaitumiwa na mpachika mabao mahiri wa klabu hiyo, Amissi Tambwe na kuitaka namba 10 ambayo amepewa Mliberia, Kpah Sherman.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mwashuiya alisema lengo kubwa la kuigomea jezi hiyo 19 na kuitaka 10 ni kutokana na mapenzi yake makubwa aliyokuwa nayo juu ya straika wa timu ya Barcelona na Argentina, Lionel Messi, ambaye amekuwa akimuiga kwa staili ya uchezaji mara nyingi.
“Kusema ukweli jezi namba 19 niliyopewa wala huwa siipendi kabisa kuitumia kutokana na mimi mapenzi yangu yapo katika jezi namba 10 ambayo nikiivaa huwa najisikia raha kabisa kutokana na kuvaliwa na ‘role model’ wangu, Lionel Messi.
“Yote tisa, kumi nimefurahi sana kusaini mkataba wa miaka mitatu ndani ya klabu kubwa kama Yanga, sasa kazi kwangu kufanya jitahada katika ushindani wa namba, si unajua kila mtu anafanya kwa lengo la kupata namba na si kitu kingine.
“Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitaishukuru timu yangu ya Kimondo kwa kunilea na kunifanya nijulikane hadi hapa nilipofikia, shukrani za dhati ziende kwao,” alisema Mwashuiya.

No comments:

Post a Comment