Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe
Magufuli kiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba
mkoani Mbeya jana katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika kwenye
viwanja vya shule ya msingi Tunduma na kuhudhuriwa maelfu ya wananchi,
Dr. John Pombe Magufuli amewaomba wananchi wa Tunduma kura za ndiyo ili
aweze kuongoza watanzania katika kupeleka gurudumu la maendeleo mbele
zaidi.
Amesema ametumikia nchi hii kwa
miaka 20 serikalini akiwa Waziri na amekuwa akisimamia kile
anachokiamini kwamba ndiyo maendeleo ya watanzania, amekuwa mkweli,
muaminifu kwa viongozi wake, mcha mungu na mchapa kazi hivyo anaomba
nafasi ya urais ili aweze kuona Tanzania yenye mabadiliko bora kwa
watanzania na siyo bora mabadiliko.
Uchaguzi mkuu wa jamhuri ya
Muungao ya Tanzania wa Rais , Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika
Oktoba 25 mwaka huu nchini kote, ambapo vyama mbalimbali vya siasa
vinatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huo(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-TUNDUMA) |
No comments:
Post a Comment