KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

August 31, 2015

GARI LA POLISI LAGONGA, KUUA MWANAFUNZI PWANI: WANANCHI WAFUNGA BARABARA KUFUATIA TUKIO HILO


Wananchi wa eneo la Misugusugu Wilayani Kibaha Mkoani Pwani hii leo wamefunga barabara baada ya Wanafunzi wawili kugongwa na gari la Jeshi la Polisi na kupelekea kifo cha Mwanafunzi Mmoja


Akiongea na Mtandao huu, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Jaffary Mohammed amesema baada ya tukio hilo Wanachi walifunga barabara kutokana na hasira ya tukio lakini jeshi la Polisi limetuliza hali na linamshikilia Dereva wa gari hilo kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda Jaffary ameongeza kuwa katika tukio hilo Mwanafunzi aliejeruhiwa amelazwa katika hospitali ya Tumbi na mwili wa marehemu upo mochwari katika hosptali hiyo.

Aidha Jaffari ameongeza kuwa kwa sasa hali ya kiusalama imetulia baada ya jeshi la polisi kutuliza hali iliyojitokeza huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi na badala yale wafuate sheria.
 
Katika hatua nyingine amewataka madereva wafate sheria za barabarani kwa kufuata alama zilizowekwa pamoja na kupunguza mwendo katika maeneo ya watu ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

No comments:

Post a Comment