KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

August 26, 2015

SALVA KIIR AKUBALI KUTIA SAHIHI MAKUBALIANO YA AMANI

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema kuwa ataweka sahihi ya makubaliano ya amani siku ya jumatano baada ya kukataa kufanya hivyo wiki iliopita.
Msemaji wa Salva Kiir amesema kuwa rais huyo ataweka sahihi yake ya makubaliano hayo katika mji mkuu wa Juba mbele ya viongozi wa eneo hili.
Salva Kiir anakabiliwa na vikwazo pamoja na kikwazo cha umoja wa mataifa cha kutonunua silaha baada ya kukataa kuidhinisha makubaliano hayo.
Mpinzani wake ambaye ndio kiongozi wa waasi Riek Machar tayari ameweka sahihi mkataba huo ili kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochukua miezi 20.

No comments:

Post a Comment