KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

August 26, 2015

VIONGOZI WATAKIWA KUZINGATIA MISINGI YA KIDEMOKRASIA KATIKA UCHAGUZI MKUU

Na Joseph Ishengoma MAELEZO, ESTONIA
.………………………………………………………

Kiongozi mmoja amewataka wanasiasa nchini kuhakikisha wanalinda amani iliyopo kwa kuweka mazingira yatakayosaidia uchaguzi ujao unafanyika kwa kufuata misingi ya kidemokrasia na utawala bora.  

Meya wa jimbo la Haaspalu, nchini Estonia, Bwana Urmas Sukles ametoa wito huo jana wakati wa mahojiano na waandishi wa habari wa Tanzania walioko kwenye ziara ya mafunzo ya wiki moja nchini Estonia.  

“Viongozi lazima wadumishe amani iliyopo kwa kufuata matakwa ya wananchi. Katika maeneo mengi duniani, wananchi wanataka viongozi waliokaribu nao, wenye uwezo wa kutatua matakwa yao na kufuata misingi ya demokrasia na utawala bora,” amesema.  

Alisema ni vizuri kwa wanasiasa kuhakikisha wanaedesha uchaguzi huo kwa misingi ya demokrasia na utawala bora kwa manufaa ya wananchi. Mwezi Oktoba mwaka huu, Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu kuchagua Rais, wabunge na madiwani.  

Bwana Sukles alisema amani katika nchi nyingi duniani inatoweka baada ya baadhi ya wanasiasa kukataa matokeo ya uchaguzi kwa madai kuwa wao ndio washindi hata kama ushaidi wa kula hunapingana na madai yao. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, ni vyema wanasiasa kukubali matokeo pindi wanaposhindwa kwenye chaguzi na kutumia kushindwa huko kujifunza wananchi wanataka nini ili wajipange upya.  

“Mwanzoni mwa miaka ya 1990, Mimi niliwahi kuwa Meya katika mji huu kwa miaka tisa, nikaingia tena kwenye uchaguzi nikashindwa nikapumzika kwa kipindi kimoja na baadaye nikarudi tena na kuchaguliwa. Kipindi nilichokuwa nje ya madaraka nilijifunza wananchi wanataka nini, ndio maana nishiriki tena katika uchaguzi na nikashinda” alisema.  

Katika hatua nyingine Meya huyo wa mji wa Haapsalu alishauri serikali kutumia teknolojia wakati wa mchakato wa kupiga na kuhesabu kura katika uchaguzi mkuu na kueleza jinsi Estonia inavyotumia teknolojia wakati wa zoezi la kupiga na kuhesabu kura bila kusababisha manunguniko miongoni mwa wagombea na wafuasi wao.  

Alisema kupiga kura kwa njia ya mtandao kunaokoa muda, kunaimarisha demokrasia, kunasaidia watu kufanya maamuzi sahihi na pia kunarahisisha zoezi hilo.  

"Watu wengi wana simu zenye ‘intaneti’ kwa hiyo ni rahisi kwao kupiga kura kwa haraka badala ya kupoteza muda kwenda vituoni kupiga kura. Halafu unaweza kupiga kura zaidi ya mara moja, lakini kura ya mwisho ndiyo inayohesabiwa kwa hiyo mtu ana uwezo wa kubadili uamuzi wake bila kuathiri uchaguzi kwasababu namba yake ya kitambulisho cha kupigia kura inatokea mara moja tu,” alisema. 
  
Asilimia 98 ya wakati wa Estonia wanatumia huduma ya mtandao wa internet(wIfI) bure jambo linalorahisisha maendeleo kukua kwa kasi.

No comments:

Post a Comment