![]() |
Wakati shule zote za umma na binafsi
zikianza kufungwa kuanzia hii leo nchini Kenya, Rais wa nchi hiyo Uhuru
Kenyatta akihutubia taifa hilo kwa njia ya televisheni amesisitiza kuwa
serikali ya nchi hiyo haina uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara
wanayodai waalimu wanaoendelea na mgomo.
Ametoa wito mgogoro huo kutatuliwa kwa amani na kusema kuwa shule zote zinafungwa kuanzia leo.Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu ukiendelea. Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za umma na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi nyumbani. Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu. |
September 21, 2015
KENYATTA: HATUWEZI KULIPA WAALIMU MSHAHARA HUO!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment