KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 21, 2015

HAMISI KIIZA ‘DIEGO’ SASA ‘AWANYIMA USINGIZI’ YANGA SC…NA ANA HASIRA NAO KINOMA!

Hamisi Friday Kiiza 'Diego' sasa anawanyima usingizi Yanga SCNa Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
HAT TRICK ya kwanza ya msimu ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imetoka kwa mshambuliaji Mganda, Hamisi Friday Kiiza maarufu kama Diego.
Kiiza alifunga mabao matatu jana Simba SC ikishinda 3-1 dhidi ya timu ngumu, Kagera Sugar ya Bukoba Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na sasa Simba SC inakwenda kambini Zanzibar kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC wikiendi hii hapo hapo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tangu jana mashabiki wa Yanga SC wameanza kumuhofia Kiiza baada ya kuona na kusikia habari zake dhidi ya Kagera Sugar, hususan wakikumbuka alikuwa mchezaji wao.
Kiiza aliichezea Yanga SC kwa miaka minne kabla ya kutemwa mwaka jana na kocha Mbrazil, Marcio Maximo ambaye alifukuzwa mwaka huo huo, nafasi yake ikichukuliwa na Mholanzi, Hans van der Pluijm.
Mashabiki wa Yanga SC hawakuridhishwa na kitendo cha kuachwa kwa Kiiza, lakini waliamua kukubali yaishe na mchezaji huyo akarejea kwao Uganda kupumzika.
Baada ya takriban nusu msimu wa kutokuwa na timu, Kiiza ameibukia kwa mahasimu Simba SC ambao walimsajili baada ya kumuuza mshambuliaji wao mwingine Mganda, Emmanuel Okwi.Zaidi tembelea Bin Zubeiry Blog

No comments:

Post a Comment