![]() |
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ na mzazi mwenzake Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’
wakimtoa mtoto wao, Latiffah Nasibu 'Princes Tiffah'.
YAMETIMIA! Baada ya kutoonekana sura kwa zaidi ya siku 40 tangu azaliwe, hatimaye mtoto wa mkali wao ndani ya Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Latifah ‘Tiffah’ ameonekana hadharani (live), Ijumaa Wikienda linakuwa la kwanza kuripoti.
Diamond na Tiffah
Tukio hilo la kihistoria kwa Diamond na mzazi mwenzake Zarina Hassan
‘Zari The Boss Lady’ lilichukua nafasi jana, nyumbani kwake
Madale-Tegeta jijini Dar. Waandishi wetu, Musa Mateja na Imelda Mtema
waliokuwepo kwenye tukio hilo mwanzo-mwisho waliripoti live Makao Makuu
ya gazeti hili, Bamaga-Mwenge:Saa 7 mchana MAANDALIZI Makao Makuu: Mateja na Imelda mbona kimya nini kinaendelea huko? Imelda: Mkuu huku mambo ndiyo yameiva, maandalizi ni bab’kubwa, pamepambwa pakapambika kila sehemu. Ongea na Musa huyu hapa… Musa Mateja: Hapa nawaona watoto wa ‘kaswida’ wakianza kwa utangulizi wa nyimbo za kumtukuza Mungu. Mkuu…Mkuu…ngoja nikuunganishe na Imelda naona ana kitu anataka kukujuza…Zaidi tembelea Global Publishers |
September 21, 2015
KWA MARA YA KWANZA TIFFAH LIVE!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment