KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 2, 2015

MBATIA AMJIBU DKT SLAA,ASEMA ANATAKA KUWATOA KWENYE RELI ILI WAANZAE KUJIBIZANA NAYE

Mwenyekiti mwenza wa UKAWA James Mbatia (Pichani) amezungumza  mchana huu na Waandishi wa habari na kujibu baadhi ya mambo aliyosema Dkt.Wilbroad Slaa Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Slaa, Dkt Slaa katika hotuba yake aliuponda uamuzi wa Chadema wa kumsimamisha Waziri Mkuu wa zamani Mhe.Edward Lowassa, alisema Lowassa si mfasi na hafai kuwa Rais wa Tanzania.
 Mbatia alisema "Napenda kuwaomba Watanzania tusimame wote kupata Katiba mpya ambayo ndiyo ajenda ya mgombea wetu Lowassa".
Mbatia aliwaomba Watanzania waelewe UKAWA tunasimamia utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji ndani ya Tanzania.
Alisema Wanasiasa hasa wale wa CCM Mwakyembe na Sita, wanaotaka midahalo waje waongee na mimi wasimsumbue Mgombea wetu Lowassa sio saizi yao.
  "Hivi ni viashiria kwamba CCM wameshindwa hoja, mara kuleta mambo ya udini, mara wanaibua hili mara lile. wanataka kuchafua amani yetu kwa kuigiza masuala ya dini," alisema
Alisema "Tukisema tuibue masuala yote na kashifa za kuuzwa kwa nyumba, kuna mtu atabaki salama? 
Dondoo za Mbatia wakati akizungumza na vyombo vya habari lei
Mbatia: Eti Lowassa akija ndani ya Ukawa atakuja na Wenyeviti wa CCM..hakuwahi kusema..kayasemea wapi?
Mbatia: Wewe unasema ni muadilifu ulipewa Milioni 500 mwaka 2008 unakuja kusema leo baada ya miaka 7? Tuwe wakweli.
Mbatia: Eti suala la rushwa zaidi ya miaka 7 usiripoti halafu uje useme leo, kusema uongo ni kazi sana.
Mbatia: Napenda kuwaomba watanzania wote ambao ni zaidi ya milioni 46, wasiruhusu nchi yetu ikaharibiwa na watu 100.
Mbatia: Wakenya walisema hata kama ana makosa, walisema huyo huyo tunamtaka, wakampigia kura na leo ni Rais wao.
Mbatia: Watu wachache wanaotaka eti kwa lolote lile lazima waendelee kubaki madarakani, tunasema hapana.
Mbatia: Lazima tufute mfumo huu uondoke tuwe na Tanzania mpya.
Mbatia: Napenda kuwaomba wale Viongozi wa dini walionewa kwa yale ya jana, wasamehe na waachane nayo.
Mbatia: Lowassa hajawahi kutamka kuwa nikija ndani ya UKAWA nitakuja na wabunge 50, wenyeviti wa CCM na Makatibu nk.
Mbatia: Kama hana faida haya mafuriko tungepata wapi? Nyota ya Lowassa inang'aa hata wafanye nini hawamuwezi huyu jamaa
Mbatia: Hatuna haja ya kuanza kumjadili, hiyo ni kulipasua Taifa la Tanzania kwa maslahi binafsi
Mbatia: Kilichotusikitisha ni yeye kuhusisha watu wengine wasiohusika kwenye jamii yetu, viongozi wa dini wenye heshima zao, acha sisi vyama vya siasa tusuguane wenyewe.
Mbatia: Zimebaki siku 50 na kitu, haki itendeki na nchi yetu ibaki na amani siku zote
Mbatia: Anasema kaja kupambana na Lowassa kwakuwa anagombea urais, sasa Sumaye naye anagombea urais?
Mbatia: Nimesoma barua ya ufisadi, ufisadi ni mfumo na Lowassa ana haki ya kujielezea lakini hawa wanataka kututoa kwenye reli tuanze kujibizana mmoja na wengine.

No comments:

Post a Comment