![]() |
| Papa Francis akikaribishwa Marekani na Rais Barack Obama |
Kiongozi wa Kanisa
Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Marekani katika siku ya
kwanza ya ziara ya kihistoria nchini humo ambapo amelakiwa na Rais wa
nchi hiyo Barack Obama.
Papa Francis aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Andrew Air Force Base kutoka nchini Cuba.
Huku
Marekani ikiwa na zaidi ya waumini wa Katoliki wapatao milioni sabini
ziara hiyo ya papa inaoneka kuwa tukio kubwa nchini humo.
Kiongozi
huyo wa kidini ambaye anaitembelea Marekani kwa mara ya kwanza atafanya
ziara na kuongoza ibada katika miji ya Washington, New York na
Philadelphia.
Wakati Papa Francis akiondoka nchini Cuba Papa
Francis aliwaambia waandishi wa habari kuwa yeye sio muumini wa mlengo
wa kushoto kama wengi wanavyodhani.
Papa alisema hatazungumzia
suala la vikwazo vya biashara kati ya Cuba na Marekani, licha ya
kuchukua nafasi muhimu katika mazungumzo ambayo yamesababisha mahusiano
ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kurejeshwa mapema mwaka huu.



No comments:
Post a Comment